#Business

MWENYEKITI WA KQ KIPRONO KITTONY AJIUZULU KUTOKA BODI YA NSE

Mwenyekiti mpya wa Bodi ya Shirika la Ndege la Kenya (KQ) Kiprono Kittony amejiuzulu kutoka bodi ya Soko la Hisa la Nairobi (NSE). Kittony anaondoka katika bodi ya NSE baada ya kuhudumu kwa takriban miaka sita tangu 2020.

Kuondoka kwake kunafuatia kuteuliwa kwake Machi 1, 2026, kama mwenyekiti mpya wa shirika la ndege la Kenya Airways, ambapo amemrithi Michael Joseph, ambaye alistaafu kutoka wadhifa huo.

Wakati wa uongozi wake katika NSE, Kittony alisimamia maendeleo kadhaa muhimu katika soko la mitaji, ikiwa ni pamoja na toleo kubwa la awali la umma la Kenya (IPO) kupitia uuzaji wa hisa katika Kampuni ya Kenya Pipeline (KPC).

Imetayarishwa na Maurine Amwayi

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *