#Football #Sports

NYABERI BADO ANA MATUMAINI YA KUPANDA DARAJA

Kocha wa Fortune Sacco FC, Vincent Nyaberi, amesema timu yake bado ina nafasi nzuri ya kupanda daraja kutoka Ligi ya National Super League licha ya kushika nafasi ya sita kwenye msimamo wa jedwali.

Nyaberi amesema bado wana matumaini ya kumaliza miongoni mwa timu tatu bora ifikapo mwisho wa msimu. Matumaini hayo yaliimarika Jumamosi baada ya Fortune Sacco kukomesha mechi tatu mfululizo bila ushindi kwa kuichapa vikali timu mpya ya Kabati Youth FC katika uwanja wa St Sebastian Park.

Kwa sasa timu hiyo yenye makao yake Murang’a inashikilia nafasi ya sita kwenye msimamo wa ligi ikiwa na pointi 36 baada ya kucheza mechi 23.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *