ORERO AAHIDI KUSAIDIA WAFANYABIASHARA WA TOI MARKET
Mbunge wa Kibra Peter Orero ameahidi kuwasaidia wafanyabiashara waliopoteza riziki zao kufuatia moto ulioteketeza vibanda katika soko la Toi Jumatatu asubuhi.
Katika taarifa yake, Orero ameeleza mshikamano wake na wafanyabiashara walioathirika akisema soko hilo ni uti wa mgongo wa uchumi wa eneo hilo na chanzo muhimu cha mapato kwa wakazi wengi.
Mbunge huyo pia amesema wanafunzi wa Shule ya Msingi ya Toi waliruhusiwa kuondoka mapema kama tahadhari wakati moto ukiendelea, akisisitiza kuwa shule hiyo haikuwa katika hatari na hatua hiyo ilichukuliwa kwa sababu za usalama pekee.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 









































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































