#Local News

UPASUAJI WA MIILI YA KERICHO KUFANYWA

Zoezi la upasuaji wa miili 32 iliyofukuliwa kutoka kaburi la pamoja kwenye kaunti ya Kericho hapo jana linatarajiwa kuanza muda wowote ili kubaini chanzo cha vifo vya waathiriwa hao wasiojulikana, huku ikiibuka kuwa huenda miili hiyo ilisafirishwa kutoka hospitali ya rufaa ya kaunti ya Nyamira.

Kulingana na mwanapatholojia wa serikali Dakta Richard Njoroge, miili 7 ni ya watu wazima huku 25 ikiwa ya watoto wachanga, ikionyesha dalili za kutoka kwenye makafani na hospitalini.

Kulingana na uchunguzi wa awali, hospitali hiyo ilikuwa imepewa amri ya mahakama kuzika miili 13 katika kaburi la umma kwenye kaunti ya Kericho.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *