SWAZURI NA WENZAKE WAACHILIWA HURU KWENYE KESI YA ARDHI
Mahakama ya hakimu imemuachilia huru aliyekuwa mwenyekiti wa Tume ya Kitaifa ya Ardhi, Mohammed Abdalla Swazuri, pamoja na washitakiwa wengine kadhaa katika kesi ya ardhi iliyokuwa ikifuatiliwa kwa karibu.
Watu 17 walikuwa wakishtakiwa kwa njama na fidia isiyo halali ya ardhi ya Shirika la Reli la Kenya yenye thamani ya shilingi milioni 221.
Katika uamuzi wake, mahakama imesema upande wa mashtaka haukuthibitisha kesi yake bila shaka yoyote, na hivyo Swazuri pamoja na wenzake wakaachiliwa huru baada ya kukana mashtaka ya matumizi mabaya ya ofisi, ulaghai na utakatishaji wa fedha.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 









































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































