110: IDADI YA VIFO KUTOKANA NA MAFURIKO
Idadi ya watu waliofariki kutokana na mafuriko yaliyosababishwa na mvua kubwa nchuini imepanda na kufikia watu 110 kufikia jana jioni, serikali ikisema hali inaendelea kuwa mbaya katika maeneo ambako mvua hiyo inaendelea.
Kwenye taaifa ya hivi punde, wizara ya usalama wa kitaifa imesema kuwa kaunti 30 zimeathirika kufikia sasa, Kilifi, Bungoma, Kirinyaga, Nyeri, Kiambu, Uasin Gishu na Mandera zikiwa za hivi punde.
Kaunti ya Nairobi pekee imeripoti vifo 37, serikali ikiwataka wananchi kushirikiana kwa kutoa taarifa za majanga na kuchukua tahadhari za mapema.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 









































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































