IEBC YAANZA USAJILI MPYA WA WAPIGA KURA
Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC), imetangaza kuanza kwa zoezi la Usajili Endelevu wa Wapiga Kura ulioboreshwa, huku ikibainisha baadhi ya maeneo yatakayoachwa nje ya zoezi hilo la kitaifa.
Kupitia taarifa iliyochapishwa kwenye ukurasa wake wa X tume hiyo imesema zoezi hilo la siku 30 tayari limeanza na litakamilika Aprili 28,likilenga kuongeza idadi ya wapiga kura kabla ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2027.
IEBC imeeleza kuwa zoezi hilo halitafanyika katika maeneo yenye chaguzi ndogo au kesi za uchaguzi zinazoendelea, yakiwemo wadi za Porro na Endo pamoja na maeneo ya Emurua Dikirr, Malava na Mbeere Kaskazini, ili kuepusha kuathiri michakato ya uchaguzi inayoendelea.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 









































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































