WAATHIRIWA WA MAANDAMANO WATAKA MUDA ZAIDI
Huku zikiwa zimesalia siku 2 kabla ya kukamilika kwa muda waliopewa waathiriwa wa maandamano kuwasilisha stakabadhi hitajika ili kuzingatiwa kwa fidia, familia za waathiriwa hao zimeitaka tume ya kitaifa kuhusu haki za kibinadamu kuziongeza muda zaidi.
Miongoni mwa malalamishi ya familia hizo ni ukosefu wa mawasiliano ya kutosha pamoja na njia mwafaka za kuifikia tume hiyo.
Mkutano wa jana kati ya waathiriwa hao na tume hiyo ulifutiliwa mbali dakika za mwisho.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 









































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































