KENYA YALIPA ADA YA AFCON
Baada ya wiki kadhaa za kutokuwa na uhakika, Kenya imelipa ada ya kuandaa Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) yenye thamani ya dola milioni 30 (Sh3.9 bilioni),
Waziri wa Michezo, Salim Mvurya, amesema kuwa nchi imetekeleza mahitaji yote yaliyowekwa na Shirikisho la Soka Afrika (CAF).
Aidha ameongeza kuwa serikali imepanga upya Kamati ya Kuandaa Mashindano (LOC) ikijumuisha wataalamu kutoka sekta ya umma na binafsi ili kuimarisha uwezo wa taasisi kabla ya mashindano.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 









































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































