JIJI KAVU: MAJI KUPOTEA NAIROBI WIKI IJAYO
Uhaba wa maji unatarajiwa katika mengi ya maeneo ya jiji la Nairobi kuanzia Jumatatu ijayo, baada ya shirika la Athi Water Works Development kufunga mfumo wake muhimu kukamilisha ujenzi.
Kupitia notisi ya umma, kampuni ya maji ya Nairobi City Water imesema mfumo huo utafungwa kuanzia tarehe 6 hadi 11 mwezi huu.
Miongoni mwa maeneo yatakayoathirika ni pamoja na Riverside, Parklands, Lavington, Kileleshwa, Mamlaka Road na viunga vya maeneo hayo.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 









































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































