FIFA U17 WC: STARLETS WAJIANDAA MAZOEZINI
Kikosi cha chipukizi wa timu ya taifa ya soka ya wanawake Junior Starlets kimeimarisha mazoezi yake kinapojiandaa kwa mechi ya kufuzu mashindano ya FIFA U17dhidi ya Namibia, kinapolenga kurejea katika mashindano hayo ya kimataifa.
Kikosi hicho kilichofanya mazoezi yake katika uwanja wa Kasarani jana, kitachuana na Namibia kwenye mikondo miwili, tarehe 12 na marudiano tarehe 18 mwezi huu.
Kocha mkuu Mildred Cheche, amesema kudumishwa kwa wachezaji wa kikosi chake kunawaweka katika hali nzuri, wachezaji kadhaa wakidumishwa katika kikosi kilichoandikisha rekodi mwaka jana.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 









































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































