#Football #Sports

MIKWAJU YA PENLATI YAOKOLEA ARSENAL, ATLETICO

Julian Alvarez aliirejesha Atletico Madrid mchezoni kupitia mkwaju wa penalti katika mechi ya mkondo wa kwanza ya awamu ya semi fainali za dimba la klabu bingwa bara Ulaya jana usiku dhidi ya Arsenal na kuishia sare ya bao 1.

Viktor Gyokeres aliwaweka viongozi wa EPL kifua mbele kunako dakika ya 44 vile vile kupitia mkwaju wa penalti baada ya kuangushwa katika eneo la hatari, ila Atletico wakapewa mkwaju wa penalti baada ya Ben White kuunawa mpira kwenye lilo hilo katika kipindi cha pili.

Hata hivyo, Arsenal walighadhabishwa na hatua ya VAR kufutilia mbali mkwaju mwingine wa penalti dakika za mwisho baada ya David Hancko kuonekana kumchezea visivyo nguvu mpya Eberechi Eze.

Atletico walibuni nafasi kadhaa katika kipindi cha pili na kuihemesha Arsenal, ila wakakosa makali ya kumalizia ambayo huenda wakajutia iwapo watabanduliwa katika mechi ya marudiano Jumanne wiki ijayo.

Mshindi wa pambano hilo atangojea mshindi wa pambano la Jumatano baina ya Bayern na PSG ila kumenyana kwenye fainali jijini Budapest, nchini Hungary.

Kabla ya hapo, Arsenal watakabaliana na Fulham wikendi hii wanapowania taji la EPL na Manchester City, nao naye kocha mkuu wa Atletico Diego Simeone akiwa na fursa ya kuwapumzisha wachezaji wake nguzo ikizingatiwa kuwa hawana kikubwa cha kuchezea katika ligi ya La Liga ambayo huenda Barcelona wakaondoka nayo.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

MIKWAJU YA PENLATI YAOKOLEA ARSENAL, ATLETICO

HAKIMI NJE DHIDI YA BAYERN

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *