UKUAJI WA UCHUMI WA KENYA WAPUNGUA HADI ASILIMIA 4.6 MWAKA 2025
Shirika la kitaifa kuhusu takwimu, KNBS, limesema kuwa ukuaji wa uchumi wa Kenya ulishuka hadi asilimia 4.6 mwaka 2025 kutoka asilimia 4.7 mwaka 2024, kwa sababu ya utendaji dhaifu katika sekta za kilimo na utengenezaji.
KNBS imesema kwamba ukuaji katika sekta za kilimo, misitu na uvuvi ulipungua hadi asilimia 3.1 mwaka 2025, kutoka asilimia 4.4 mwaka uliopita. Ukuaji wa polepole ulichangiwa kwa kiasi kikubwa na mifumo tofauti ya hali ya hewa ya mwaka mzima, mvua za muda mrefu na muda mfupi zilizo juu au chini ya wastani, na kusababisha uzalishaji tofauti wa mazao.
Shirkika hilo aidha limebainisha kuwa ukuaji wa sekta ya utengenezaji uliongezeka kwa asilimia 2, ikilinganishwa na ukuaji wa asilimia 3 wa mwaka 2024. Wakati huo huo, ukuaji katika sekta ya usafirishaji na uhifadhi ulipungua hadi asilimia 3.7 kutoka asilimia 4.3 mwaka 2024.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 









































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































