UTOAJI WA CHANJO YA ROTAVIRUS KUTATIZIKA
Wizara ya afya imetangaza kwamba utoaji wa chanjo za rotavirus zinazotumiwa kwa chanjo ya kawaida ya Watoto utatatizika kwa muda kutokana na uhaba wa chanjo hizo nchini.
Kupitia tangazo, Waziri wa afya Aden Duale, amefichua uhaba wa chanjo hizo, ambazo hutolewa kwa Watoto wanapofikisha umri wa wiki 6, 10 na 14, shehena ya chanjo hizo iliyochelewa ikitarajiwa nchini mwezi ujao.
Chanjo hiyo hutumiwa kuwakinga Watoto dhidi ya kuendesha, kutapika na kuishiwa na maji mwilini.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 










































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































