TUZO YA BALLON D’OR KUFANYIKA LONDON

Sherehe za utoaji wa tuzo ya Ballon d’Or mwaka 2026 zitafanyika kwa mara ya kwanza jijini London Oktoba 26 kuadhimisha miaka 70 tangu tuzo hiyo ilipotolewa kwa mara ya kwanza mwaka 1956. Waandalizi wamesema hafla hiyo itaadhimisha kumbukumbu ya mwanasoka wa Uingereza Stanley Matthews aliyekuwa mshindi wa kwanza wa tuzo hiyo. Katika miaka ya hivi karibuni, tuzo […]

WAMOTO AIPA KABRAS NAFASI YA KUTWAA ENTERPRISE CUP

Kocha wa raga wa Chuo Kikuu cha Kibabii Peter Wamoto ameipa Kabras RFC nafasi kubwa ya kutwaa taji la Enterprise Cup katika fainali itakayochezwa Jumamosi kwenye uwanja wa RFUEA Grounds. Kabras wanapania kutwaa ubingwa huo kwa mara ya sita mfululizo baada ya hivi karibuni kutwaa taji la Kenya Cup kwa mara ya tano mtawalia huku wakikabiliwa na […]

STARLETS YAJIANDAA KWA MECHI DHIDI YA UGANDA

Beki wa timu ya taifa ya wanawake chini ya umri wa miaka 17 Pauline Namisi pamoja na mshambuliaji Emily Adhiambo wamesema timu hiyo itategemea ukomavu, nidhamu ya kiufundi na sapoti ya mashabiki katika mechi ya marudiano dhidi ya Uganda. Wachezaji hao wameeleza kuwa sare ya mabao 1-1 waliyoipata katika mechi ya kwanza iliyochezwa katika uwanja […]

MOTO WAZUKA SHULE YA GACHARAGE MURANG’A

Moto ulizuka usiku wa Alhamisi katika shule ya upili ya Gacharage eneo la Kandara Ruchu Kaunti ya Murang’a na kuzua hofu mpya kuhusu usalama wa taasisi za elimu nchini. Tukio hilo limejiri saa chache baada ya mkasa wa moto katika shule ya Utumishi Girls Academy eneo la Gilgil uliosababisha vifo vya wanafunzi 16 na kujeruhi wengine wengi […]

MAHAKAMA YASITISHA MPANGO WA KITUO CHA EBOLA

Mahakama Kuu imesitisha kwa muda mpango wa serikali wa kuanzisha au kuendesha kituo chochote cha karantini, kutenga au kutibu Ebola nchini Kenya chini ya makubaliano yoyote na Marekani au serikali nyingine za kigeni. Mahakama pia imezuia serikali kuwaruhusu kuingia nchini, kuwapokea au kuwahamisha watu waliothibitishwa au wanaoshukiwa kuathiriwa na virusi vya Ebola hadi kesi hiyo […]

HUZUNI GILGIL BAADA YA MOTO WA SHULE, DNA KUFANYWA

Maumivu na simanzi vilitawala katika shule ya Utumishi Girls Academy eneo la Gilgil huku wazazi na walezi wakihangaika kutafuta taarifa za watoto wao kufuatia moto uliosababisha vifo vya wanafunzi 16 na kujeruhi wengine 79. Msemaji wa Serikali Isaac Mwaura amesema mwanapatholojia wa serikali Johansen Oduor tayari amewasili eneo hilo kuanza uchunguzi wa vinasaba vya DNA […]

RUTO AZINDUA MPANGO WA KUPUNGUZA VIFO VYA KINA MAMA NA WATOTO WACHANGA

Rais William Ruto amezindua rasmi mpango wa kitaifa wa EWENE wa miaka 2026 hadi 2028 unaolenga kupunguza vifo vya kina mama wajawazito na watoto wachanga nchini. Mpango huo unalenga kuboresha huduma za afya, kuimarisha uwajibikaji pamoja na kutekeleza afua maalum katika kaunti zinazorekodi visa vingi vya vifo vya kina mama na watoto wachanga. Serikali pia imeanzisha mpango […]

RUTO: WALIO NA MISHAHARA YA CHINI YA SH30,000 WASILIPISHWE KODI

Rais William Ruto ametangaza kuwa serikali itapeleka bungeni pendekezo la kuwaondoa wafanyakazi wanaopata mshahara wa hadi shilingi elfu 30 katika ulipaji wa kodi ya mapato. Akizungumza katika kikao cha Kitaifa cha Maombi jijini Nairobi, Ruto amesema hatua hiyo inalenga kupunguza ugumu wa maisha kwa wananchi wa kipato cha chini licha ya serikali kukabiliwa na upungufu wa mapato […]

BUNGE LAHOJI BAJETI YA 2026/27

Wanachama wa Kamati ya Bajeti na Matumizi ya Fedha wameibua wasiwasi kuhusu upungufu wa mapato, uwajibikaji katika sekta ya afya pamoja na shinikizo la kifedha wakati wa kupitia bajeti ya mwaka wa fedha 2026/27. Waziri wa Hazina ya Kitaifa John Mbadi ametetea bajeti ya shilingi trilioni 4.785 yenye nakisi ya shilingi trilioni 1.111 itakayofadhiliwa hasa […]

MASWALI YAIBUKA KUHUSU MOTO WA SHULE YA UTUMISHI

Maswali yanaendelea kuibuka kuhusu chanzo cha moto ulioteketeza bweni katika shule ya Utumishi Girls Academy iliyoko Kaunti ya Nakuru huku Wakenya wengi wakieleza hofu kuhusu usalama wa wanafunzi katika mabweni ya shule. Taarifa mpya zinaashiria kuwa huenda moto huo uliosababisha vifo vya wanafunzi 16 na kujeruhi wengine 79 uliwashwa kimakusudi, jambo ambalo limeongeza wasiwasi miongoni […]