PVK YAKOSOA SIASA ZA MATUSI MIONGONI MWA VIONGOZI
Muungano wa Pentecostal Voice of Kenya ukiongozwa na Mwenyekiti wake ambaye pia ni Kiongozi wa Kanisa la Jesus Teaching Ministry Apostle Peter Manyuru umekosoa kuongezeka kwa utamaduni wa matusi na uhasama wa kisiasa miongoni mwa viongozi, ukionya kuwa hali hiyo inachochea mgawanyiko na kudhalilisha hadhi ya uongozi wa umma.
Katika taarifa kwa vyombo vya habari, muungano huo umeeleza wasiwasi kuwa viongozi wa serikali na upinzani wanajihusisha na mivutano ya hadharani badala ya kushughulikia mahitaji ya wananchi, ukitaja hali hiyo kuwa hatari na inayoweza kuandaa mazingira ya chaguzi zenye taharuki.
Muungano huo umetaka kukomeshwa mara moja kwa siasa za matusi na kuwataka viongozi kuzingatia maadili, uwajibikaji na kuhudumia wananchi.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 










































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































