MUSEVENI AONGOZA MATOKEO YA AWALI UGANDA

Rais mkongwe wa Uganda, Yoweri Museveni, ameongoza kwa mbali katika matokeo ya awali ya uchaguzi wa urais, huku kukiwa na taarifa kinzani kuhusu visa vya vurugu vilivyoripotiwa baada ya kura kupigwa. Kwa mujibu wa matokeo yaliyotangazwa na tume ya uchaguzi, Museveni ana asilimia 76.25 ya kura kulingana na kura zilizohesabiwa kutoka karibu nusu ya vituo vya […]

OMTATAH APINGA UFADHILI WA SHIF

Seneta wa Kaunti ya Busia, Okiya Omtatah, ameiambia Mahakama Kuu kuwa huduma ya afya kwa wote inapaswa kufadhiliwa moja kwa moja kupitia kodi, akisisitiza kuwa ni wajibu wa kikatiba wa serikali kuhakikisha wananchi wanapata huduma za afya bila kutozwa ada au michango ya ziada Omtatah anadai kuwa Mfuko wa Bima ya Afya ya Jamii, SHIF, […]

TUKIO LA POLISI LAZUA HASIRA NANDI HILLS

Wakenya wameonyesha hasira zao baada ya klipu ya CCTV iliyosambaa mitandaoni kuonyesha maafisa wa polisi wenye silaha wakiwashambulia vijana waliokuwa wakicheza pool katika mji wa Nandi Hills, huku viongozi sasa wakitaka hatua za haraka zichukuliwe dhidi ya waliohusika. Seneta wa Nandi, Samson Cherargei, pamoja na Mbunge wa Embakasi Mashariki, Babu Owino, wamelaani vikali kitendo hicho walichokitaja […]

KENYA YATARAJIA UKUAJI WA MAUZO YA NJE BAADA YA MAKUBALIANO YA KIBIASHARA NA CHINA

Serikali kuu imesema inatarajia ukuaji wa mauzo ya nje baada ya China kutoa asilimia 98.2 ya soko la ushuru sifuri kwa bidhaa kutoka nchi hiyo chini ya makubaliano ya kufuta ushuru yaliyotangazwa hivi karibuni. Waziri wa uwekezaji, biashara, na viwanda Lee Kinyanjui amesema hatua hiyo muhimu inafuatia makubaliano kati ya nchi hizo mbili baada ya China […]

MOROCCO NA SENEGAL KATIKA FAINALI YA AFCON

Wenyeji Morocco na Senegal wamefuzu fainali ya kombe la mataifa ya afrika baada ya ushindi wa jasho katika mechi za nusu fainali zilizochezwa jumatano. Morocco walitinga fainali baada ya kuibuka na ushindi wa mikwaju ya penalti dhidi ya Nigeria kufuatia sare ya bila kufungana katika nusu fainali iliyochezwa Rabat. Fainali hiyo inawakutanisha mataifa mawili yanayoongoza […]

WAITHIRA NA AMBANI WATWAA TUZO ZA FKF DECEMBER

Nahodha wa Murang’a seal Joe Waithira ametangazwa mchezaji bora wa ligi kuu ya FKF kwa mwezi wa desemba 2025 baada ya kiwango bora wakati wa sikukuu. Waithira aliwashinda Ovella Ochieng’, Tyson Otieno, Paul Okoth, Jimmy Owili na Bixente Lizarazu, baada ya kufunga mabao manne katika mechi tatu, akiisaidia Murang’a seal kukusanya pointi saba kati ya […]

HARAMBEE STARLETS KWA KUNDI GUMU WAFCON 2026

Harambee Starlets wamepangwa katika kundi a lenye ushindani mkali kwenye kombe la mataifa ya afrika kwa wanawake 2026 litakalofanyika Morocco kuanzia machi 17 hadi aprili 2. Kwa mujibu wa droo iliyofanyika alhamisi katika kituo cha soka cha Mohammed vi mjini Rabat, Kenya itakutana na wenyeji Morocco, Senegal na algeria. Mashindano ya mwaka 2026 yataandika historia […]

KeNHA YATANGAZA KUFUNGWA KWA BARABARA KUU YA UHURU

Mamlaka ya barabara kuu ya kitaifa nchini KENHA imetangaza kufungwa kwa muda kwa sehemu muhimu za barabara kando ya barabara kuu ya uhuru katika mzunguko wa haile selassie avenue ili kurahisisha kazi muhimu za barabara. Katika taarifa ya umma, KENHA imetangaza awamu ya i ya kufungwa kwa huduma wakati wa saa za usiku zisizo  nne usiku hadi saa kumi na […]

UMEME KUKATIKA KAUNTI YA NYERI

Kampuni ya kusambaza umeme nchini  imetangaza kukatika kwa umeme hii leo katika sehemu tofauti za kaunti ya Nyeri kuanzia saa tatu asubuhi hadi saa kumi na moja jioni. Baadhi ya maeneo yatakayo athirika ni  gachatha, wamagana, na kariguini. Imetayarishwa na Antony Nyongesa

WANAFUNZI WA GREDI YA 10 KUONGEZEWA MUDA

Wizara ya elimu inataka kuongeza muda kwa wanafunzi wanaojiunga na gredi ya 10 ikisisitiza kuwa itafikia asilimia 100 ya mpito. Hili linajiri baada ya takriban wanafunzi 400,000 pekee kati ya wanafunzi milioni 1.1 waliowekwa kuripoti shuleni. Ingawa shule za kitaifa zimerekodi zaidi ya asilimia 90 ya wanafunzi waliojitokeza, mamia ya maelfu ya wanafunzi bado wamesalia  nyumbani huku wazazi wakikabiliana na gharama huku wasiwasi kuhusu uhaba wa vifaa ukiongezeka. […]