#Local News

CHANGAMOTO ZA CBE ZAKATIZA NDOTO

Mfumo wa umilisi wa masomo, CBE unaendelea kukumbwa na changamoto huku maelfu ya wanafunzi wa Junior Secondary wakiripotiwa kuacha shule hali inayotia wasiwasi kuhusu utekelezaji wa mfumo mpya wa elimu nchini.

Wadau wa elimu wanasema sababu kuu ni ukosefu wa miundombinu ya kutosha gharama za masomo pamoja na uhaba wa walimu wenye ujuzi maalum wa kufundisha katika ngazi hiyo mpya.

Ripoti inaonyesha kuwa baadhi ya wazazi wanashindwa kumudu gharama zinazohusiana na mahitaji mapya ya junior secondary huku wengine wakilalamikia umbali wa shule zilizoandaliwa kupokea wanafunzi hao.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *