UHASAMA WANUKIA DIAMOND LEAGUE
Bingwa wa dunia katika mbio za wanawake za mita 3,000 Faith Cherotich ameratibiwa kufufua uhasama wake dhidi ya mkenya mwenzake anayekimbilia taifa la Bahrain Winfred Mutile Yavi watakapokutana na mbio ya kuruka viunzi na maji kwenye mashindano ya pili ya Diamond League jijini Xiamen baadaye mwezi hu.
Wawili hao watakutana kwa mara ya 12 katika kipindi cha misimu 4, na ikiwa ni mara ya kwanza tangu wamenyane katika mbio za World Championships jiji Tokyo Septemba mwaka jana ambako Cherotich alimpiku Yavi.
Mkenya huyo mwenye umri wa miaka 21 aliibuka bingwa katika mbio hizo na rekodi mpya ya 8:51.59.
Wawili hao wametamalaki mbio za kuruka viunzi na maji katika miaka ya hivi karibuni, wakishinda mataji 3 ya Diamond League na mataji 12 ya mbio hizo za Diamond League yakigawanywa miongoni mwao katika misimu 3 iliyopita.
Cherotich ni bingwa wa dunia na katika mbio za Wanda Diamond League, akishinda mbio hizo mwaka wa 2024 na 2025.
Naye Yavi ni bingwa mtetezi wa olimpiki na mwanamke wa pili mwenye kasi zaidi katika historia ya mbio za mita 3000 ya kuruka
Beatrice Chepkoech.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 




























































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































