WAFANYAKAZI TRANS NZOIA WATISHIA MGOMO
Huku wafanyakazi nchini wakijiunga na wenzao kote ulimwenguni kuadhimisha siku ya kimataifa ya wafanyakazi, Leba Dei, mmungano wa wafanyakazi wa umma katika kaunti ya Trans Nzoia umetishia kushiriki mgomo na kusambaratisha shughuli zote za utoaji huduma ikiwa wanachama wake hawatalipwa mshahara wa miezi miwili.
Mwenyekiti wa wafanyakazi hao Lennox Opicho na mwenzake wa muungano wa wauguzi (KNUN) Cyprian Nyakundi wanasema wafanyakazi wanapitia changamoto tele kwa kiwango cha kutokidhi mahitaji ya kimsingi yakiwemo chakula, na pia kutatizika kufika kazini.
Hata hivyo, gavana George Natembeya, amesema hatua hiyo imetokana na serikali kuu kuchelewesha mgao wa kaunti.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 



















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































