#Local News

 SERIKALI YAJICHANGANYA NA MAFUTA

Maswali yameibuka kuhusu uamuzi wa serikali kutangaza kwamba itaagiza mafuta ya viwango vya chini kwa muda wa miezi 6 ijayo hadi Oktoba mwaka huu, ikizingatiwa kuwa maafisa 3 katika sekta ya kawi walikamatwa na kulazimika kujiuzulu baada ya kuagiza mafuta yasiyokidhi viwango hapa nchini.

Kupitia taarifa, waziri wa biashara na viwanda Lee Kinyanjui, amesema uamuzi wa kuagiza mafuta hayo yenye viwango vya juu vya Sulphur imechochewa na misukosuko inayoshuhudiwa Mashariki ya kati na hivyo changamoto katika upatikanaji wa mafuta yenye viwango vya juu vya ubora, hatua inayohofiwa kusababisha uhaba nchini.

Kulingana na wataalam, kiwango cha juu cha Sulphur kwenye mafuta kinaathiri mazingira na magari.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *