#Local News

MAFURIKO YATATIZA UCHUKUZI NCHINI

Shughuli za usafiri katika maeneo mbali mbali ya nchi ikiwemo jijini Nairobi zimeendelea kutatizika kutokana na mvua kubwa ambayo imesababisha barabara kufurika maji, mbali na na nyumba kadhaa kufurika.

Miongoni mwa barabara hizo ni ile ya Mombasa Road ambako sehemu kadhaa kama vile Belle Vue na GM zimefurika maji na kusababisha msongamano kwenye barabara hiyo kutokana na mwendo wa pole pole wa magari.

Idara ya hali ya anga imetabiri mvua kubwa kuendelea katika mengi ya maeneo huku mengine yakitarajia mvua ya viwango vya wastani kufikia kesho.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *