IEBC YAWEKA WAZI IDADI YA SAJILI WAPYA
Wakenya ambao hawakusajiliwa katika zoezi endelevu la usajili wa wapiga kura wapya lililokamilika mapema wiki hii wametakiwa kufanya hivyo katika afisi za tume huru ya uchaguzi na mipaka IEBC katika maeneo bunge.
Hii nii baada ya zoezi hilo kukamilika huku tume hiyo ikisema jumla ya wapiga kura wapya 2, 612,725 tangu usajili wa kitaifa ulipozinduliwa.
Eneo la Bonde la ufa linaoongoza kwa wapiga kura wapya ambao ni 671,958 na kufuatiwa na Central likiwa na 399,220 nalo eneo la Magharibi likiwa na wapiga kuya wapya 231,168.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 





























































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































