COTU YAISHINIKIZA SERIKALI KUHUSU MIKATABA YA KAZI
Katibu Mkuu wa COTU Francis Atwoli ameongeza shinikizo kwa Rais William Ruto kuharakisha kuridhia mikataba miwili muhimu ya kimataifa ya kazi, akionya kuwa kuchelewa kunadhoofisha ulinzi wa wafanyakazi pamoja na ahadi za serikali
Akizungumza katika maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi kaunti ya Vihiga, Atwoli amesisitiza umuhimu wa serikali kuipa kipaumbele mikataba ya Shirika la Kazi Duniani, ikiwemo Mkataba wa 189 na 190
Ameeleza kuwa mikataba hiyo inalenga kulinda wafanyakazi wa majumbani pamoja na kukabiliana na vitendo vya ukatili na unyanyasaji mahali pa kazi, changamoto alizosema zimeenea na zinahitaji hatua za haraka kutoka kwa serikali.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 




























































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































