MUTUA AELEZA MAFANIKIO YA AJIRA WAKATI WA MAADHIMISHO YA SIKU YA LEBA
Waziri wa Leba Alfred Mutua amesema kumekuwa na mafanikio makubwa katika sekta ya ajira nchini, akibainisha kuwa mamilioni ya nafasi za kazi zimezalishwa katika sekta mbalimbali.
Akizungumza wakati wa maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi katika kaunti ya Vihiga, Mutua amesema utumishi wa umma umeunda ajira milioni 1.895 huku sekta ya biashara ndogo na za kati ikichangia ajira milioni 2.1
Aidha, sekta ya hoteli imezalisha ajira milioni 1.5, viwanda ajira 443,000, uchukuzi na mawasiliano ajira 75,000 na ujenzi ajira 50,000, akisisitiza kuwa serikali inaendelea kuweka mikakati ya kuongeza nafasi za kazi zaidi kwa wananchi.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 




























































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































