BLADES WAJIANDAA KWA WIKENDI NGUMU BAADA YA MAANDALIZI KUHARIBIKA
Kocha mkuu wa timu ya Strathmore Blades Tony Ochieng amesema maandalizi ya timu yake kuelekea mechi za Ligi Kuu ya Mpira wa Kikapu kwa Wanaume nchini Kenya wikendi hii hayajakuwa mazuri kutokana na changamoto za hali ya hewa.
Ochieng amesema timu imefanikiwa kufanya mazoezi moja pekee, huku wapinzani wao wakinufaika na kufanya mazoezi kwenye viwanja vya ndani visivyoathiriwa na mvua, Akiongeza kuwa atakosa kikosi kamili kutokana na majeraha na baadhi ya wachezaji kuwa na majukumu binafsi.
Hata hivyo, kocha huyo amesema bado ana matumaini kuwa timu yake itaonyesha kiwango kizuri licha ya changamoto hizo.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 




























































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































