#uncategorized

AMBANI: LEOPARDS BADO KATIKA MBIO ZA UBINGWA

Kocha mkuu wa AFC Leopards Fred Ambani amesema klabu hiyo bado iko kwenye mbio za ubingwa wa Ligi Kuu ya Kenya licha ya kuwa nyuma ya vinara Gor Mahia kwa pointi sita.

Leopards kwa sasa wako nafasi ya pili wakiwa na Alama 55, kufuatia kipigo cha bao 1–0 katika mchezo wa Mashemeji Derby wiki iliyopitaAmbani akisema bado wana mechi zilizobaki na endapo wapinzani wao watapoteza pointi, wana nafasi ya kupindua matokeo.

Aidha, ratiba ya timu hiyo imeathiriwa baada ya mechi yao ya ugenini dhidi ya Ulinzi Stars kuahirishwa kutokana na majukumu ya Kombe la Mozzart Bet Ambani aKIsema mabadiliko hayo yana changamoto lakini yanaweza pia kuwasaidia kujipanga upya kimwili na kiakili.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *