MUDAVADI AUNGA MKONO RUTO 2027, ASISITIZA AWAMU MBILI
Mkuu wa Mawaziri Musalia Mudavadi amesema kuwa tayari alionyesha mwelekeo wa kisiasa katika uchaguzi uliopita na kuwa msimamo huo bado haujabadilika kuelekea uchaguzi wa 2027.
Mudavadi amesisitiza kuwa njia ni ile ile, akieleza wazi kuwa anamuunga mkono Rais William Ruto kuendelea kuongoza kwa muhula mwingine.
Ameongeza kuwa ana imani kuwa Ruto atahudumu kwa mihula miwili, akiwataka wafuasi kuungana na kuhakikisha azma hiyo inafanikishwa kupitia mshikamano wa kisiasa na uungwaji mkono wa wananchi.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































