MAADALIZI YA CHAN YAKAMILIKA
Waziri wa Michezo Salim Mvurya amehitimisha ziara yake ya mwisho ya ukaguzi kabla ya Michuano ya Ubingwa wa Mataifa ya Afrika (CHAN) 2024, akionyesha imani katika utayari wa Kenya kuandaa mashindano hayo yanayofanyika kila baada ya miaka miwili.
Mvurya alikagua uwanja Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta (JKIA) ambapo alikagua itifaki za kuwasili na vifaa vilivyowekwa kwa wajumbe watakao zuru nchi.
Akizungumza baada ya ukaguzi huo, Mvurya alibainisha kuwa ameridhishwa na mipangilio na miundo msingi iliyopo, akisema Kenya iko tayari kukaribisha timu na maafisa watakaoshiriki. Mapema wiki mvurya alikua ametembelea viwanja vya Nyayo na Kasarani, viwili kati ya viwanja muhimu vya michuano ya CHAN 2024. Alipongeza maendeleo na ubora wa kazi iliyofanyika katika viwanja vyote viwili.
Mvurya alisema kuwa litakuwa jukumu la pamoja kwa wananchi kuhakikisha kwamba tunaandaa michuano hiyo yenye mafanikio.Harambee Stars ikiendelea kuimarisha maandalizi yake kuelekea michuano ya CHAN 2024.
Wakati huohuo Bunge FC, timu inayoundwa na Wabunge, Maseneta na wafanyakazi wa Tume ya Utumishi ya Bunge, iliipa timu hiyo motisha ya ziada kuelekea mechi ya ufunguzi wakiitunuki shillingi Ksh.1 milioni ili kuwapa motisha kabla ya michezo ya bara hilo.
Imetayarishwa na Nelson Andati
English 




























































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































