SENETI KUAMUA HATMA YA MUTAI WIKI IJAYO
Gavana wa Kericho Eric Mutai atabaini hatma yake ya kubanduliwa kutoka afisini mwishoni mwa mwezi huu, wakati seneti itajadili hoja hiyo kwa kipindi cha siku 3.
Spika wa seneti Amason Kingi, amemwagiza karani wa bunge hilo kuhakikisha gavana Mutai na wawakilishi wadi waliomng’atua mamlakani wiki iliyopita wanapata mwaliko wa kuhudhuria vikao vya kusikiliza hoja hiyo.
Aidha, amemtaka gavana huyo na wawakilishi wadi kuwasilisha stakabadhi muhimu za hoja hiyo bungeni kufikia Jumanne wiki ijayo.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 




























































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































