#Local News

MARAGA ATAKA EACC KUICHUNGUZA SHA

Aliyekuwa jaji mkuu David Maraga  anataka tume ya kupambana na ufisadi Eacc kupewa nafasi ya kuendesha uchunguzi katika fedha zilizodaiwa kupotea kupitia malipo kwa  vituo bandia vya afya kupitia mamlaka ya SHA.

Maraga ambaye amezidi kukosoa jinsi mfumo wa SHA unavyotekelezwa anasema kumekuwa na juhudi za kuficha ukweli kuhusu  mamilioni ya fedha zilizopotea.

Maraga amepuuzilia mbali hakikisho kutoka kwa waziri wa afya kuwa vituo vilivyojihusisha na ulaghai vilifungwa.

Imetayarishwa na Maureen Mukhobe.

MARAGA ATAKA EACC KUICHUNGUZA SHA

UHC NJIA PANDA KUHUSU UHAMISHO

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *