BUNGE LAFUTILIA MBALI VIKAO VYA LEO
Bunge limefutilia mbali vikao vyake vya leo ili kuwawezesha wabunge kuhudhuria ibada ya wafu kutoa heshima zao za mwisho kwa aliyekuwa mwenzao wa Emurua Dikirr Johana Ng’eno, aliyefariki Jumamosi na watu wengine watano kwenye ajali ya ndege.
Kiongozi wa walio wengi bungeni Kimani Ichung’wa, aliweka wazi tangazo hilo wakati wa vikao vya jana, akisema hatua hiyo itawapa wabunge fursa ya kumwomboleza mwenzao.
Mbunge huyo atazikwa Ijumaa katika eneo bunge lake.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 




























































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































