RUTO APOKEA MABALOZI WATATU NCHINI
Rais William Ruto amepokea hati za utambulisho za mabalo watatu ambao wameteuliwa katika Ikulu ya Nairobi ikiwa ni kuashiria mwanzo wa kazi zao za kidiplomasia nchini.
Watatu hao ni pamoja na Rulan Mahmoud Samara wa Jordan, Jacinto Januario Maguni wa Mozambique na Saad Bin Abdullah Alnofaia wa Saudi Arabia.
Ruto amewahakikishia mabalozi hao ushirikiano kamili wanapoanza majukumu yao huku akionyesha imani ya ushirikiano kati ya pande hizo mbili.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 




























































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































