#Local News

EACC YAINUA MJELEDI

Tume ya maadili na kukabili ufisadi, EACC, imewataka makatibu wakuu katika wizara zote na maafisa wengine wakuu serikalini kujiepusha na kampeni za kisiasa jinsi wanavyohitajika kisheria.

Tume hiyo imeonya kuwachukulia hatua za kisheria maafisa watakaokiuka sheria hiyo, onyo yao ikijiri huku makatibu wakuu na maafisa wengine wakionekana hadharani kwenye mikutano ya kisiasa na kufanya kampeni.

Maafisa wa EACC walikuwa wakizungumza walipofika mbele ya kamati ya bunge kuhusu utekelezaji wa katiba.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

EACC YAINUA MJELEDI

SERIKALI YAKADIRIA UKUAJI WA UCHUMI

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *