DUALE: SHA INAWAHUDUMIA WALIMU
Waziri wa afya Aden Duale amekana kuwepo kwa changamoto kubwa kwa walimu kupata matibabu chini ya bima ya afya SHA, akisisitiza kuwa walimu zaidi ya 249,000 na watu wengine wanaowategemea wakiwemo Watoto wa walimu hao wametibiwa chini ya bima hiyo.
Duale amehakikisha kuwa changamoto za awali katika utekelezaji wa mpango huo zinaendelea kushughulikiwa ili kufanikisha utoaji huduma za matibabu chini ya SHA bila matatizo.
Kauli yake inajiri huku walimu wakitoa makataa ya siku 7 kutatuliwa kwa changamoto hizo la sivyo wagome.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 




























































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































