IEBC YAONYA KUHUSU UTAPELI WA AJIRA
Tume huru ya uchaguzi na mipaka, IEBC, imetoa tahadhari kwa umma kuhusiana matangazo ya ulaghai yanayosambazwa kwenye mitandao ya kijamii kuhusu nafasi za ajira katika tume hiyo.
Kupitia tangazo, IEBC imefafanua kwamba matangazo hayo ni ya udanganyifu, na kusisitiza kwamba nafasi za ajira katika tume hiyo hutolewa tu kupitia tovuti yake rasmi.
Imewataka wakenya kuwa macho dhidi ya matapeli.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 




























































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































