#Football #Sports

USIKU MKUBWA ULAYA, MECHI ZA AWAMU YA 16

Ni usiku mwingine wa kinyang’anyiro cha klabu bingwa bara Ulaya ambapo jumla ya mechi 4 za raundi ya 16 zitachezwa leo usiku, huku nyingine 4 zikisakatwa hapo kesho, ukiwa ni mkondo wa kwanza.

Liverpool watarejea kikaangoni nchini Uturiki kumenyana na Galatasaray, walikocharazwa bao 1-0 katika awamu ya makundi msimu huu.

Mechi nyingine itajumuisha Newcastle, ambao wataialika Barcelona huku Atletico Madrid wakiwa wenyeji wa Tottenham.

Atalanta, mwakilishi wa pekee wa Italia katika kipute hicho, watasakata dhidi ya miamba wa Ujerumani, Bayern Munich.

Mkondo wa mwisho utachezwa wiki ijayo ili kusaka tiketi ya kuingia robo fainali.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

USIKU MKUBWA ULAYA, MECHI ZA AWAMU YA 16

RODRI APIGWA FAINI, APONEA MARUFUKU

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *