#Business

SEHEMU YA BANDARI YA MOMBASA KUBINAFSISHWA, SERIKALI

Serikali kuu iko katika hatua ya mwisho ya kuwezesha sehemu za Bandari ya Mombasa na Lamu kusimamiwa na mashirika ya kibinafsi.

Serikali imepanga kufuta sheria ya mamlaka ya bandari ya Kenya, KPA, ili kuondoa mamlaka hiyo na kuibadilisha kuwa Kampuni ya Umma yenye Hati ya Hisa (PLC) chini ya Sheria ya Kampuni, hatua ambayo itarahisisha uwekezaji wa sehemu ya Bandari ya Mombasa na gati tatu za Bandari ya Lamu.

Kwenye hati ya Mwisho ya Uwazi wa Ushirikiano wa Umma na Sekta Binafsi (PPP) katika Sekta ya Bandari ya Kenya, imebainika serikali inalenga kuongeza mapato ya bandari za Mombasa na Lamu kwa Sh44 bilioni kila mwaka.

Imetayarishwa na Maurine Amwayi

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *