#Local News

MBUNGE KIBAGENDI ADAI KUTISHWA BAADA YA KUZUNGUMZIA UFISADI

Mbunge wa Kitutu Chache Kusini Antony Kibagendi sasa anadai anakabiliwa na vitisho katika kile anachosema ni juhudi za kumnyamazisha kufuatia madai yake kuhusu ufisadi katika Wizara ya Afya.

Kibagendi anadai kuwa mashirika ya serikali kama vile Tume ya Maadili na Kupambana na Ufisadi (EACC) pamoja na Idara ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) yametumiwa dhidi yake.

Mbunge huyo amesema kuwa msimamo wake wa mara kwa mara wa kutaka uwajibikaji katika usimamizi wa Mamlaka ya Afya ya Jamii (SHA) pamoja na wito wake wa kukomesha ufisadi bungeni, umewakasirisha baadhi ya watu wenye ushawishi ambao sasa wanamlenga.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *