MAADHIMISHO YA NAKURU RFC YAVUTIA MAKUMI YA TIMU
Zaidi ya timu 40 za mchezo wa raga zimeratibiwa kushiriki mashindano ya 10-aside yatakayoandaliwa na kalbu ya Nakuru RFC mapema mwezi ujao, klabu hiyo itakapokuwa ikiadhimisha miaka 100 tangu kuanzishwa kwake.
Klabu hiyo imehusishwa na mchango wake mkubwa kwa raga ya Kenya, ikiwemo kuwatoa wachezaji mahiri wanaochezea timu ya taifa.
Mashindano hayo huandaliwa kila mwezi Aprili, na timu mbili kutoka Uganda na Sudan zimeratibiwa kushiriki Makala yam waka huu.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 




























































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































