#Local News

MAHAKAMA YASIMAMISHA FAINI ZA PAPO HAPO


Waendeshaji magari nchini wamepata afueni baada ya mahakama kuu kusimamisha utekelezaji wa mfumo wa mamlaka ya usalama barabarani, NTSA, kuwatoza faini za papo hapo wanapovunja sheria za trafiki.

Kwenye uamuzi mapema leo, jaji Bahati Mwamuye ameizuia NTSA na afisi ya mwanasheria mkuu dhidi ya kutekeleza mfumo wa kuwatoza faini waendeshaji magari kwa njia yoyote ile hadi kesi iliyowasilishwa itakaposikilizwa na kuamuliwa.

Kesi hiyo iliwasilishwa na shirika la Sheria Mtaani, linalohoji kuwa mfumo huo unatoza faini baini ya kubaini kosa moja kwa moja bila onyo, au hata kuangaziwa na mtu.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

MAHAKAMA YASIMAMISHA FAINI ZA PAPO HAPO

EACC, NG-CDF ZAJADILI KUZIBA UFISADI

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *