TUJU AAPA KUPIGANI ARDHI ILIYONADIWA
Aliyekuwa katibu mkuu wa chama cha Jubilee Raphael Tuju, amesisitiza kuwa hatalegeza juhudi za kupigania kipande chake cha ardhi cha ekari 27 kilicho mtaani Karen jijini Nairobi, licha ya kupigwa mnada.
Kwa mujibu wa mbunge huyo wa zamani, kiasi cha fedha anazodaiwa na benki moja ni kidogo mno ikilinganishwa na thamani ya ardhi hiyo.
Ameibua madai kwamba mkopo huo umeingizwa siasa.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 




























































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































