#Business

BEI ZA PETROLI, DIZELI, NA MAFUTA TAA KUSALIA ZILIVYO – EPRA

Ni afueni kwa mwananchi baada ya mamlaka ya mafuta na udhibiti wa nishati nchini EPRA kutangaza kuwa Bei za mafuta ya petroli, dizeli na mafuta ya taa hazitaongezwa katika ukaguzi wa hivi punde kati ya Machi 15, 2026 hadi Aprili 15, 2026.Hii ina maana kwamba, jijini Nairobi, lita moja ya petroli itaendelea kuuzwa kwa Ksh.178.28, huku dizeli ikiuzwa kwa Ksh. 166.54 na Mafuta ya Taa kwa Ksh. 152.78 kutumika kwa siku 30 zijazo.

Mjini Mombasa, gharama itasalia kuwa Ksh.175.00 kwa lita moja ya petroli, Ksh.163.26 ya dizeli na Ksh.149.49 kwa mafuta taa mtawalia.Mjini Nakuru, Super Petrol itauzwa kwa Ksh.177.34, Dizeli Ksh.165.95, na Mafuta ya Taa Ksh.152.21.

Wakati huo huo, wateja jijini Kisumu watanunua lita moja ya petroli kwa bei ya Ksh.178.16, dizeli kwa Ksh.166.76 na mafuta ya taa kwa Ksh.153.03. Mwezi uliopita, bei ya petroli ilishuka kwa Ksh.4.20, dizeli kwa Ksh.3.90 na mafuta taa kwa Ksh.1.00 kwa lita.

Imetayarishwa na Maurine Amwayi

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *