#Local News

RUTO ASUTA UPINZANI WAKATI WA ZIARA MAGHARIBI

Rais William Ruto amewashutumu viongozi wa upinzani akisema hawana ajenda madhubuti kwa Wakenya akidai kuwa hawajawasilisha mpango wowote unaolenga kuboresha maisha ya Wakenya.

 Akizungumza wakati wa ziara yake katika eneo la Magharibi mwa nchi, Rais amesema baadhi ya wanasiasa wanajihusisha zaidi na siasa badala ya kutoa suluhu kwa changamoto zinazowakabili wananchi

Ziara ya Rais katika eneo la Magharibi inatarajiwa kudumu kwa siku tatu ambapo atakagua utekelezaji wa miradi mbalimbali ya serikali ikiwemo miundombinu ya barabara pamoja na mpango wa nyumba za bei nafuu.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *