SAKAJA AAGIZA MPANGO WA SAA 48 KUKABILI MAFURIKO NAIROBI
Gavana wa Nairobi Johnson Sakaja ameagiza kuandaliwa kwa mpango wa hatua za saa 48 ili kukabiliana na mafuriko, matatizo ya mifereji ya maji na uharibifu wa miundombinu katika jiji la Nairobi.
Agizo hilo lilitolewa baada ya mkutano wa dharura uliofanyika katika City Hall uliowaleta pamoja maafisa wa serikali ya kaunti na mashirika ya serikali ya kitaifa ukilenga kujadili hali mbaya ya mafuriko inayoshuhudiwa jijini kufuatia mvua kubwa zinazoendelea kunyesha tangu Machi 6.
Sakaja pia amewaagiza maafisa kuandaa ripoti itakayobainisha maeneo hatarishi ya mifereji ya maji, kutambua barabara na miundombinu iliyoharibika, pamoja na kueleza kazi zinazohitajika kufanywa, mashirika yatakayohusika na gharama za matengenezo ili ukarabati uanze mara moja.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 




























































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































