#Business

NCPB YACHUKUA KAZI YA RUZUKU YA MBEGU KUTOKA KAMPUNI YA MBEGU

Bodi ya Kitaifa ya Nafaka na Mazao (NCPB) imeagizwa kuwajibika kwa mpango wa ruzuku ya mbegu ya mahindi kutoka kwa Kampuni ya Mbegu, kufuatia kikao cha Kamati ya Bunge ya Kilimo na Mifugo tarehe 16 mwezi huu.

Hatua hiyo inalenga kurahisisha usambazaji wa mbegu za ruzuku katika msimu wa upanzi unaoendelea na kuhakikisha wakulima wanapata pembejeo kwa wakati. Mwenyekiti wa Kamati John Mutunga ameagiza NCPB kutumia mfumo wake uliopo wa usambazaji wa mbolea, ambao husajili wakulima kulingana na ukubwa wa shamba na kufanya kazi na kaunti kwa utoaji wa mwisho, ili pia kudhibiti ruzuku ya mbegu.

Agizo hilo linafuatia ucheleweshaji wa utekelezaji wa ruzuku ya mbegu ya mahindi. Wiki iliyopita, Katibu Mkuu wa Kilimo Kipronoh Ronoh alitoa waraka unaoitaka Kampuni ya Kenya Seed kutoa mbegu za mahindi zinazofadhiliwa kwa shilingi 250 kwa kilo, na bei iliyopunguzwa kwa kiasi kikubwa, ikiungwa mkono na  nyongeza kutoka kwa bajeti yam waka wa 2025/2026 ya shilingi bilioni mbili.

Imetayarishwa na Maurine Amwayi

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *