RUTO AZINDUA UJENZI WA RELI YA KISASA YA SGR
Rais William Ruto amezindua rasmi ujenzi wa reli ya kisasa ya SGR kutoka Naivasha kuelekea Kisumu na Malaba, baada ya kuweka jiwe la msingi katika viwanja vya Chuo cha Ualimu cha Narok.
Mradi huo wa urefu wa kilomita 475 unatarajiwa kupita katika maeneo ya Naivasha, Narok, Bomet, Kericho, Nyamira, Kisumu hadi mpaka wa Malaba.
Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Rais amesema mradi huo utabadilisha uchumi wa nchi, akibainisha kuwa si tu kuhusu ujenzi wa reli bali ni hatua ya kuunganisha biashara katika ukanda wa Afrika Mashariki na kuiweka Kenya kama lango kuu la kibiashara katika eneo hilo.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 




























































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































