VIJANA WATARAJIA AJIRA ZA SGR
Mamia ya vijana nchini wanatarajiwa kunufaika na nafasi za ajira kwenye mradi wa ujenzi wa awamu ya pili ya reli ya kisasa, SGR, kutoka Naivasha kuelekea Malaba kupitia Kisumu ambao umeratibiwa kukamilishwa ndani ya miaka 2.
Akizungumza baada ya kuzindua mradi huo wa shilingi bilioni 500, Rais William Ruto amesema kuwa reli hiyo itarahisisha usafirishaji wa mizigo na abiria kuelekea Magharibi mwa nchi.
Reli hiyo itajengwa awamu 2 za 2B na 2C, 2C ikitoka Narok hadi Kisumu huku 2B ikipita Kisumu, Siaya, Vihiga, Kakamega hadi Busia.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 




























































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































