KINDIKI AJIBU GACHAGUA KUHUSU UHALIFU WA MERU
Naibu Rais Kithure Kindiki amejibu kauli za mtangulizi wake Rigathi Gachagua kufuatia onyo la siku kumi alilotoa kuhusu kukomesha uhalifu wa kutumia silaha katika eneo la Meru Kaskazini, kaunti ya Meru.
Kauli hiyo ya Kindiki inajiri baada ya Gachagua kutishia kuhamasisha wakazi wa maeneo yanayokumbwa na mashambulizi hayo kujihami iwapo serikali haitachukua hatua ndani ya muda uliowekwa.
Kindiki amemtupia lawama Gachagua akidai kuwa alishindwa kukabili tatizo hilo alipokuwa mamlakani, na kwamba hana msingi wa kumkosoa kuhusu hali ya sasa ya usalama.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 




























































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































