#Football #Sports

BB BREAD FC KUKABILIANA NA KENYA POLICE KWENYE FKF CUP

Klabu ya BB Bread  italazimika kucheza kwa kiwango cha juu ikiwa wanataka kufuzu hatua ya robo fainali ya FKF kwa mara ya tatu mfululizo, baada ya kuteuliwa kukabiliana na Kenya Police katika raundi ya 16, kulingana na droo iliyofanywa kwenye Uwanja wa Taifa wa Nyayo.

Bread FC tayari wameiondoa AFC Leopards na Gor Mahia kufikia hatua hii na watahitaji kucheza bila doa ikiwa wanataka kuondoa Police kwenye mashindano.

Droo hiyo pia imethibitisha mechi kadhaa kati ya timu za Ligi Kuu ya Kenya: Tusker FC itakabiliana na Kariobangi Sharks, Kakamega Homeboyz wakikaribisha Ulinzi, na Posta Rangers watapokea mabingwa Nairobi United,

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *